sl

Paul Rand Be Identified Playground

Thursday, February 23, 2012

KARIBU DAR CALVARY TEMPLE (DCT) TABATA SHULE

KARIBU DAR CALVARY TEMPLE (DCT) TABATA SHULE Tunafurahi mno umepata nafasi ya kusali nasi leo! Ahsante kalvary ni kanisa linalowaunganisha watu wa tamaduni tofauti hapa Dar ili kumwabudu mungu kwa pamoja, mahali hapa utajifunza kweli kuu za kibiblia ambazo ukizitendea kazi zitabadili maisha yako. Hapa kalvary tunayaka pawe mahali ambapo kila anayekuja atapata nafasi ya ushirika na mungu kisha na watu wengine watakaopenda na kukuhudumia. Basi uwe huru! karibu ufurahie maisha yale ambayo mungu ameyaanda kwa ajili yako. jiunge nasi katika kipindi cha kusifu na kuabudu ushirikiane na waimbaji wa sifa kumwabudu mungu. Furahia mahuiri na mafundisho ya mafafanuzi ya maandiko yatakayobadilisha maisha yako daima.
 Taratibu za ibada zetu
Jumapili saa 1:00 - 3:00 English service saa 3:00 - 4:00 Uanafunzi saa 4:00 - 6:00 Ibada ya kiswahili
 NB: ibada ya kiingereza itaanza tarehe 5 february 2012 Wasiliana nasi: Mchungaji kiongozi - Rev Ron Swai 0767 520 968, 0784 520 968 Wasaidizi-Mch. Mwakasege - 0754 296 774(msimbazi-shemasi zetu) Mch. Tchaku- 0762 936 133(sifa na vijana)
 TUPO TABATA SHULE ILIYOKUWA TAG. GALILIYA

Wednesday, February 1, 2012

WALIOKOKA WAKIOMBEWA NA WAZEE WA KANISA LA (DCT)

Waumini waliofika katika Kanisa la Assemblies of God kanisa la Dar Calvary Temple (DCT) Tabata Shule wakiombewa baada ya kuokoka katika Ibada kubwa iliyofanyika katika viwanja wa (DCT).

MCHUNGAJI REV.RON SWAI AKIWA NA WAZEE WA KANISA WA KVCC- KIRUMBA MWANZA.

Mchungaji kiongozi Rev. Ron Swai wa kanisa la Dar Calvary Temple(DCT) akiwa na Wazee wa Kanisa wa KVCC- Kirumba Mwanza katika picha ya pamoja

SHIKA YA YESU BAND WALITIKISA KWA KUMSIFU MUNGU

Band ya Shika ya Yesu ilikuwa ni kivutio katika kumwimbia Bwana katika Kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) ilikuwa ni siku iliyompenda Mungu kwa matukio mema.

MAHUBIRI YAKIENDELEA (DCT)

Waumini wakiwa makini kumsikiliza Mhubiri ambaye hayupo pichani.

WAUMINI KATIKA PICHA (DCT) NA KVCC- KIRUMBA MWANZA.

Wazee wa Kanisa DAR CALVARY TEMPLE (DCT) na Wazee wa kanisa wa KVCC KIRUMBA MWANZA katika picha katika matukio mbalimbali katika viwanja vya Dar Calvary Temple (DCT) Tabata Shule

KWAYA YA KVCC - KIRUMBA MWANZA KATIKA KUABUDU

Kwaya ya KVCC Kirumba Mwanza ikimsifu Mungu kwa Mapambio, Mchungaji Kiongozi Rev. Ron Swai akitoa Neno kwa waumini walifika katika Ibada katika Kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) - Tabata Shule.

WAGENI WETU KUTOKA KVCC- KIRUMBA MWANZA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

Picha za Watumishi wakiwa pamoja kwa ajili ya maombi nje ya viwanja vya Dar Calvary Temple - Tabata Shule Jijini Dar es Salaam ilikuwa ni siku ya ushindi rehema za Mungu katika viwanja hivi.

KVCC -KIRUMBA MWANZA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

Wapendwa kutoka KVCC- Kirumba Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya misa kubwa iliyofanyika katika Kanisa la Dar Calvary Temple - Tabata Shule Dar es Salaam.

KVCC- KIRUMBA MWANZA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

Wageni waliotembelea DCT kutoka KVCC- Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya kufany Uinjilisti kwa kuhubiri Mitaani hapa wakiwa katika Picha ya pamoja katika misa iliyofanyika katika viwanja vya DCT Tabata Shule.

MUDA WA KUSHUKA BARAKA KWA WAUMINI.

Waumini wakiombewa kwa ajili ya Baraka za Familia zao katika ibada kubwa kabisa kufanyika katika Viwanja vya Kanisa la Dar Calvary Temple (DCT) Tabata Shule Ilala Dsm.
Mchungaji Kiongozi Rev. Ron Swai akifuatilia Mahubiri wakati wa Misa katika Viwanja vya (DCT).
Jumapili hii ilikuwa ni siku ya Kuvuna maana wapendwa wengi walipata nafasi ya kumpokea Bwana Yesu Kristo na kukiri kuwa ndiye Mwokozi wao, hapa waliokoka wakiombewa na kuingia katika maisha mapya yenye yenye matumaini. Ni katika kanisa la Assemblies of God la Dar Calvary Temple (DCT) Tabata Shule- Dar Es Salaam

MAOMBI KWA AJILI YA WATUMISHI WALIOMPOKEA BWANA YESU NA KUOKOKA


Waumini wakiendelea na Ibada Jumapili hii katika viwanja vya Kanisa la Dar Calvary Temple -Tabata Shule Jijini Dar es Salaam