MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012
KAMA ilivyo kauli mbinu ya kanisa la
Dar es Salaam Calvary Temple la Tanzania Assemblies of God kuwa kanisa hili la
DCT –Tabata shule linatekeleza kauli mbinu ya kuvuna Jiji lote la Dar Es Salaam na Ulimwengu wote, katika kutekeleza neno la Mungu Mchungaji Kiongozi Rev: Ron Swai na Wazee wa kanisa viongozi wameandaa Mkutano mkubwa katika viwanja vya DCT Tabata na kuhudhuriwa na mamia ya wapendwa.
Ni siku iliyojaa miujiza huku wapendwa wengi wakimpokea Bwana Yesu Kristo kwa kuokoka na kumpokea bwana Yesu kristo kama mwokozi wa maisha yetu, ni furaha iliyoje kwa mtu kumjua mwokozi wake, mkutano huu mkubwa wa siku tatu ulipewa jina la
GREAT GOSPEL CAMPAIGN ulianza tarehe 17-19.Feb.2012 ni mkutano ulioleta mavuno mema.
Wahubiri mahiri walihudumu katika mkutano huo walikuwa ni Askofu Lawrence Kametta na Mchungaji Rev: Ron Swai Mwl. Mashuhuri wa vyuo vya Biblia alifundisha na wapendwa kumpokea Mwokozi wetu Bwana Yesu Kristo, mafanikio ya mkutano wa Live Worship Experience katika viwanja vya DCT- Tabata Shule ni Ushindi wa kujivunia kwaWatumishi wa Mungu.
Wengi waliokoka na kuingia katika uzima wa milele ujumbe huu wenye faraja unapatikana katika maandiko matakatifu kutoka
Yohana 14:5 – 7, Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
Kila siku, kila wakati umekuwa ni muda wa miujiza katika
Kanisa hili la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) Tabata Shule. Wengi wanaokoka na kumpokea Mungu , kanisa linabarikiwa kwa kukua na kustawi na kuteka Jiji la Dar Es Salaam na Ulimwengu, nimeona fadhili za Mungu kwangu mimi
UOKOVU NI FAHARI NJOO LEO DAR ES SALAAM CALVARY TEMPLE.