sl

Paul Rand Be Identified Playground

Tuesday, May 8, 2012

RATIBA ZA MISA

  • English service Saa 3:00 - 4:00
  • Uanafunzi saa 4:00 - 4:30
  • Ibada ya kiswahili Saa 4:30 - 6:00
NB: Ibada ya kiingereza ni kila Jumapili saa 1:00 - 3:00 Asubuhi 

Wasiliana nasi: Mchungaji kiongozi - Rev Ron Swai 0767 520 968, 0784 520 968

Wasaidizi-Mch. Mwakasege - 0754 296 774(Msimamizi-shemasi zetu)

Mch. Tchaku- 0762 936 133(sifa na vijana)

TUPO TABATA SHULE ZAMANI ILIYOKUWA TAG. GALILIYA

Saturday, March 17, 2012

KARIBU DAR CALVARY TEMPLE (DCT) TABATA SHULE

KARIBU DAR CALVARY TEMPLE (DCT) TABATA SHULE Tunafurahi mno umepata nafasi ya kusali nasi leo! Ahsante kalvary ni kanisa linalowaunganisha watu wa Tamaduni tofauti hapa Dar es Salaam ili kumwabudu mungu kwa pamoja, mahali hapa utajifunza kweli kuu za kibiblia ambazo ukizitendea kazi zitabadili maisha yako. Hapa kalvary tunayaka pawe mahali ambapo kila anayekuja atapata nafasi ya ushirika na mungu kisha na watu wengine watakaopenda na kukuhudumia. Basi uwe huru! karibu ufurahie maisha yale ambayo mungu ameyaanda kwa ajili yako. jiunge nasi katika kipindi cha kusifu na kuabudu ushirikiane na waimbaji wa sifa kumwabudu mungu. Furahia mahuiri na mafundisho ya mafafanuzi ya maandiko yatakayobadilisha maisha yako daima. Taratibu za ibada zetu Jumapili saa 1:00 - 3:00 English service Saa 3:00 - 4:00 Uanafunzi saa 4:00 - 6:00 Ibada ya kiswahili NB: Ibada ya kiingereza ni kila Jumapili saa 1:00 - 3:00 Asubuhi  Wasiliana nasi: Mchungaji kiongozi - Rev Ron Swai 0767 520 968, 0784 520 968 Wasaidizi-Mch. Mwakasege - 0754 296 774(Msimbazi-shemasi zetu) Mch. Tchaku- 0762 936 133(sifa na vijana) TUPO TABATA SHULE ZAMANI ILIYOKUWA TAG. GALILIYA

Sunday, March 11, 2012

GREAT GOSPEL CAMPAGN DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012

MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012 

 KAMA ilivyo kauli mbinu ya kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple la Tanzania Assemblies of God kuwa kanisa hili la DCT –Tabata shule linatekeleza kauli mbinu ya kuvuna Jiji lote la Dar Es Salaam na Ulimwengu wote, katika kutekeleza neno la Mungu Mchungaji Kiongozi Rev: Ron Swai na Wazee wa kanisa viongozi wameandaa Mkutano mkubwa katika viwanja vya DCT Tabata na kuhudhuriwa na mamia ya wapendwa.

Ni siku iliyojaa miujiza huku wapendwa wengi wakimpokea Bwana Yesu Kristo kwa kuokoka na kumpokea bwana Yesu kristo kama mwokozi wa maisha yetu, ni furaha iliyoje kwa mtu kumjua mwokozi wake, mkutano huu mkubwa wa siku tatu ulipewa jina la GREAT GOSPEL CAMPAIGN ulianza tarehe 17-19.Feb.2012 ni mkutano ulioleta mavuno mema.

Wahubiri mahiri walihudumu katika mkutano huo walikuwa ni Askofu Lawrence Kametta na Mchungaji Rev: Ron Swai Mwl. Mashuhuri wa vyuo vya Biblia alifundisha na wapendwa kumpokea Mwokozi wetu Bwana Yesu Kristo, mafanikio ya mkutano wa Live Worship Experience katika viwanja vya DCT- Tabata Shule ni Ushindi wa kujivunia kwaWatumishi wa Mungu.

 Wengi waliokoka na kuingia katika uzima wa milele ujumbe huu wenye faraja unapatikana katika maandiko matakatifu kutoka Yohana 14:5 – 7, Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Kila siku, kila wakati umekuwa ni muda wa miujiza katika Kanisa hili la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) Tabata Shule. Wengi wanaokoka na kumpokea Mungu , kanisa linabarikiwa kwa kukua na kustawi na kuteka Jiji la Dar Es Salaam na Ulimwengu, nimeona fadhili za Mungu kwangu mimi UOKOVU NI FAHARI NJOO LEO DAR ES SALAAM CALVARY TEMPLE.

MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012

Mchungaji Kiongozi Rev: Roni Swai akifurahia wimbo unaotumbuizwa na kundi la Shika ya Yesu ambao hawaonekani katika picha hii.
Mzee wa Kanisa Frank  Narogwa akitoa maelezo na ratiba nzima katika mkutano huo katika viwanja vya DCT- Tabata Shule.

MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012

Mzee wa Kanisa Mnishi akiwakaribisha na kuwapa maelezo Wongofu wapya katika kanisa la DCT- Tabata Shule
Mwimbaji mahiri wa Muziki wa Injili nchini Jenifer Mgendi naye alikuwepo katika viwanja vya DCT - Tabata Shule akisikiliza Mahubiri yakiendelea kutoka kwa Askofu Lawrence Kametta.
Mchungaji Kiongozi Rev: Roni Swai akiwawekea mikono na kuwaombea waliokoka jioni ya Jumamosi.
Mchungaji Kiongozi Rev: Roni Swai akiwa Askofu Lawrence Kametta pamoja na Mama Askofu mama Kametta.
Mtoto akicheza kwa furaha nyimbo nzuri kutoka kwa Shika ya Yesu Band ambayo ilikuwa ni kivutio kikubwa kwa Waumini waliofika katika viwanja vya DCT- Tabata

MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012

Mchungaji Kiongozi Rev: Roni Swai akimkarisha Mama Askofu Lawrence Kametta alipowasili Kanisa la Tanzania Assemblies of God (Dar es Salaam Calvary Temple DCT - Tabata Shule)
Askofu Lawrence Kametta akitoa Neno katika Mahubiri katika Viwanja vya (DCT- Tabata Shule)
Askofu Lawrence Kametta akikemea mapepo kwa muumini aliyempokea Yesu na kukiri kuwa ndiye Mwokozi wa Maisha yake na kuachana na Shetani ndipo Mapepo yalipojitokeza na kukemewa na kumwachia huru Mtumishi wa Mungu.
Waumini wakipokea Baraka kwa maombi kutoka kwa huduma iliyotolewa katika Viwanja vya DCT - Tabata Shule
Binti aliyeokoka na kutokewa na Mapepo akipatiwa huduma na Mashemasi wa DCT - Tabata Shule.

MKUTANO WA INJILI DCT- TABATA SHULE 17- 19 Feb.2012


Waacheni Watoto waje kwangu kwa maana Ufalme wa Mbingu ni wao, hapa wanaonekana wakifurahia nyimbo kutoka kwa Waimbaji wa sifa Praise team DCT Tabata Shule.
Mchungaji Kiongozi Rev: Ron Swai akimkaribisha Askofu Lawrence Kametta kwa ajili ya Mahubiri katika Viwanja vya DCT- Tabata Shule.
Mchungaji Tchako akiabudu na kusifu na kwaya ya Praise Team DCT - Tabata Shule
Mchungaji Mwakasege akimlaki Askofu Lawrence Kametta akiwa na mkewe ambaye anasalimia na Mchungaji Kiongozi Rev: Roni Swai wakiingia katika viwanja vya (DCT) Tabata Shule